انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزخرف
السورة ٤٣

الزخرف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٦

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَـٰتِنَآ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَقَالَ إِنِّى رَسُولُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ٤٦

{46} Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema, "Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani?'" Yeye Mtukufu akabainisha hali na Musa na wito wake ambao ndio mashuhuri zaidi katika miito ya Mitume, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliutaja kwa wingi katika Kitabu chake. Aliitaja hali yake pamoja na Firauni, akasema, "Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu" zilizoashiria kwa ishara ya uhakika mkubwa usahihi wa yale aliyokuja nayo kama vile fimbo, nyoka, na kuwatumia nzige na chawa... hadi mwisho wa ishara hizo. "Aende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: 'Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!'" Aliwalingania wamkiri Mola wao Mlezi, na akawakataza kuabudu visivyokuwa Yeye.