الزخرف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
بَلْ مَتَّعْتُ هَـٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ ٢٩
{29} Na neno hili likaendelea kuwepo katika kizazi chake, amani iwe juu yake, mpaka ikawaingia anasa na dhuluma, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao" kwa matamanio ya aina mbali mbali mpaka yakawa ndiyo lengo lao na mwisho wa makusudio yao. Basi upendo wake ukiendelea kujistawisha mioyoni mwao, hadi ukawa sifa iliyoimarika ndani yake na itikadi iliyokita mizizi, "mpaka ikawafikia Haki" isipokuwa na shaka yoyote ndani yake wala mchanganyiko, "na Mtume aliyebainisha." Yaani, aliyebainisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu, na ambaye ushahidi mbalimbali ulisimama kuthibitisha ujumbe wake kwa njia angavu, kupitia tabia zake nzuri na miujiza yake, na kupitia yale aliyowasadikisha kwayo Mitume, na hata kwa wito wake tu wenyewe, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.