غافر
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَلَمَّا جَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَرِحُوا۟ بِمَا عِندَهُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ ٨٣
{83} Kisha akataja uhalifu wao mkubwa, akasema: "Mitume wao walipowajia kwa ushahidi ulio wazi" kutoka katika Vitabu vya Mwenyezi Mungu na miujiza mikubwa, na elimu yenye manufaa yenye kubainisha uongofu mbali na upotovu na haki mbali na batili, "wakajitapa kwa elimu waliyokuwa nayo" ambayo inapingana na dini ya Mitume wao. Na inajulikana vyema kuwa furaha yao hiyo inaashiria ukubwa wa kuridhika kwao nayo, kushikamana kwao nayo na uadui wao dhidi ya haki waliyokuja nayo Mitume wao, na wakaifanya batili kuwa ndiyo haki. Hili ni jambo la jumla katika elimu zote ambazo zilitumika kupinga yale ambayo Mitume walikuja nayo, ambazo aina yake inayostahili zaidi kuingizwa katika hili ni elimu ya falsafa na mantiki ya Kigiriki, ambayo kwayo aya nyingi za Qur-ani Tukufu zilikataliwa na thamani yake ikapungua katika nyoyo, na ushahidi wake wa yakini na wa uhakika mkubwa ukafanywa kuwa ushahidi wa kilafudhi tu usio na yakini yoyote, na zikatangulizwa mbele yake akili za watu wa upumbavu na ubatili. Haya ni miongoni mwa njia kubwa zaidi za kupindukia katika ishara za Mwenyezi Mungu na kuzipinga. Basi Mwenyezi Mungu ndiye tunayemuomba msaada. "Basi yakawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara." Yaani, adhabu waliyokuwa wakiifanyia mzaha ikawashukia.