انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٢

ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ خَـٰلِقُ كُلِّ شَىْءٍ لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ٦٢

{62} "Huyo" aliyefanya aliyoyafanya "ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi" aliye wa pekee katika uungu wake na aliye peke yake katika umola. Kwa sababu kuwa kwake peke yake katika neema hizi ni katika umola wake, na kuhitaji kwake kushukuriwa juu yake ni katika uungu wake. "Muumba wa kila kitu." Hili linathibitisha umola wake. "Hapana mungu ila Yeye," nalo hili linathibitisha kwamba Yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa bila mshirika yeyote. Kisha akataja waziwazi amri ya kumwabudu, akasema: "Basi mnageuzwa wapi" mkaacha kumuabudu Yeye peke Yake, bila mshirika, baada ya Yeye kuwabainishia ushahidi wa hayo na akawaangazia njia?