انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · غافر
السورة ٤٠

غافر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤

مَا يُجَـٰدِلُ فِىٓ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِى ٱلْبِلَـٰدِ ٤

{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kwamba hakuna anayebishana juu ya Aya zake isipokuwa wale waliokufuru, na kinachokusudiwa kubishana hapa ni kubishana ili kuzikanusha Aya za Mwenyezi Mungu na kuzipambanisha na batili. Hayo ni matendo ya makafiri. Ama Waumini, wao wanajisalimisha kwenye haki ili kuipindua batili kwayo. Na wala mtu asidanganywe na hali ya kidunia ya mtu na akafikiri kuwa Mwenyezi Mungu akimpa katika dunia hii ati ni ishara ya kwamba anampenda na kwamba yuko kwenye haki. Ndiyo maana akasema: "Basi kusikughuri wewe kutangatanga kwao katika nchi" wakifanya aina mbalimbali za biashara na kuchuma vitu mbalimbali. Bali la wajibu kwa mja ni kwamba awazingatie watu kwa mujibu wa haki na aangalie mambo ya kihakika ya kisheria na awapime watu kwa hayo, na asiipime haki kwa watu kama anavyofanya mtu ambaye hajui wala hata hana akili.