انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٦

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا۟ بِأَحْسَنَ مِنْهَآ أَوْ رُدُّوهَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ حَسِيبًا ٨٦

{86} Maamkizi ni kauli itokayo kwa mmoja wa wale waliokutana kwa namna ya heshima na dua, na yale yanayofungamana na usemi huo miongoni mwa uchangamfu na mfano wake. Na maamkizi ya hali ya juu kabisa ni yale yaliyoletwa kwa sheria ya salamu, kuanza na kuitikia. Kwa hivyo Yeye Mtukufu akawaamrisha Waumini kwamba wanapoamkiwa kwa aina yoyote ya maamkizi, kwamba wayaitikie kwa ya yaliyo mazuri zaidi yake kimaneno, na kwa bashasha au kwa mfano wake katika hilo. Na maana ya hilo isiyokuwa ya moja kwa moja ni katazo la kutojibu kabisa au kuiitikia kwa yaliyo chini zaidi yake. Na inachukuliwa kutoka katika Aya hii tukufu kuhimiza juu ya kuanza kusalimia, na kuamkia kwa namna mbili: Moja yake ni kwamba Mwenyezi Mungu aliamuru kwamba irudishwe kwa lililo bora zaidi au mfano wake. Na hilo linalazimu kwamba salamu inatakiwa kisheria. Na ya pili ni kile kinachoeleweka kutoka kwa vitendo vya kuboresha, nacho ni 'nzuri zaidi' kinachoashiria kushiriki salamu na kuirejesha kwa uzuri, kama ilivyo asili katika hilo. Na inatolewa katika ujumla wa Aya hii tukufu mwenye kuamkua katika hali ambayo haikuamrishwa. Kama vile yule ambaye ameshughulika na kusoma, au kusikiliza khutba, au anayeswali, na mfano wa hayo. Kwani, haitakiwi kujibu maamkizi yake. Na vile vile inatolewa katika hilo yule ambaye sheria imeamrisha ahamwe na kutomwamkua, ambaye ni muasi asiyetubia, ambaye anakomeka kwa kuhamwa. Yeye huhamwa, na wala haamkiwi, wala maamkizi yake hayaitikiwi. Na hilo ni kwa sababu (maslahi ya salamu) yanagongana na masilahi makubwa zaidi. Na inaingia katika kujibu maamkizi kila maamkizi ambayo watu wameyazoea ambayo hayakukatazwa kisheria. Basi hayo yameamrishwa kuyaitikia yayo hayo au kwa yaliyo mazuri zaidi kuyaliko. Kisha Yeye Mtukufu akaahidi mazuri na akahidi adhabu juu ya kutenda mazuri na mabaya kwa kauli yake, “Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhesabu kila kitu.” Basi huwahifadhia waja wake matendo yao mazuri yake na mabaya yake, madogo yake na makubwa yake, kisha atawalipa kulingana na kile ambacho fadhila yake inahitaji, na uadilifu wake, na hukumu yenye kusifiwa.