النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَئِنْ أَصَـٰبَكُمْ فَضْلٌ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمْ تَكُنۢ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُۥ مَوَدَّةٌ يَـٰلَيْتَنِى كُنتُ مَعَهُمْ فَأَفُوزَ فَوْزًا عَظِيمًا ٧٣
{73} Kisha akasema, “Na ikiwapata fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu” Yani nusura, na ngawira, “anasema, kana kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu na yeye: Aa! Laiti ningelikuwa pamoja nao nikafuzu kufuzu kukubwa.” Yani anatamani kuwa angekuwepo ili apate katika ngawira, na hana hamu yoyote wala nia katika kisichokuwa hilo, kana kwamba yeye si katika nyinyi, enyi kundi la Waumini. Wala hakuna baina yenu na yeye mapenzi ya kiimani ambayo katika matakwa yake ni kwamba Waumini washirikiane katika masilahi yao yote, na kuzuia madhara yao. Wanafurahia kwa kupatikana kwake hata ikiwa ni kwa mkono wa asiyekuwa yeye miongoni mwa ndugu zake Waumini, na wanaumia kwa kuikosa, na wanajitahidi wote katika kila jambo ambalo kwalo wanaitengeneza vizuri dini yao na dunia yao. Basi huyu ambaye anatamani dunia tu hana hiyo roho ya kiimani iliyotajwa.