النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ خُذُوا۟ حِذْرَكُمْ فَٱنفِرُوا۟ ثُبَاتٍ أَوِ ٱنفِرُوا۟ جَمِيعًا ٧١
{71} Yeye Mtukufu anawaamrisha waja wake Waumini kuchukua tahadhari dhidi ya maadui zao makafiri. Na hili linajumuisha kuchukua njia zote ambazo kwazo wanatafuta msaada wa kupigana nao na kuzuia hila zao na nguvu zao, miongoni mwa kutumia ngome na mahandaki, na kujifunza kurusha mishale, na kupanda, na kujifunza ufundi unaosaidia katika hilo, na yale yanayojulikana kuhusu viingilio vyao na vya kutokea vyao, na vitimbi vyao, na kwenda haraka katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kwa sababu hii, akasema, "Basi nendeni haraka katika vikosi," yani kikosi au jeshi litoke liende haraka, na lingine libaki. "Au tokeni nyote kwa pamoja." Na yote haya yanafuatana na masilahi, na kwa ajili ya kuwashinda adui, na starehe kwa Waislamu katika dini yao. Aya hii ni sawa na kauli yake Mola Mtukufu, "Na waandalieni muwezavyo miongoni mwa nguvu."