النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا ٦٥
{65} Kisha Yeye Mtukufu akaapa kwa nafsi yake kwamba hawataamini mpaka watafute hukumu kutoka kwa Mtume wake katika wanayozozana baina yao. Yani, katika kila kitu ambacho kunatokea kutofautiana ndani yake, isipokuwa masuala ya Ijmaa (makubaliano ya wanachuoni). Hayo, hayawi isipokuwa kwa kuegemezwa juu ya Kitabu na Sunnah. Kisha kutafuta hukumu huku hakutoshi mpaka uzito na dhiki viondoke kutoka katika nyoyo zao, na kwamba wanatafuta hukumu yake kwa nje na upofu tu. Kisha kutafuta hukumu yake huku hakutoshi mpaka wajisalimishe kwa hukumu yake kabisa kwa moyo mkunjufu, na utulivu wa nafsi, na kufuata kwa dhahiri na ndani. Kwa hivyo, kutafuta hukumu yake kuko katika daraja la Uislamu, na kutokuwepo na uzito kuka katika daraja la imani, na kujisalimisha kuko katika daraja la ihsani. Basi mwenye kukamilisha daraja hizi na kuzitimiza, basi kwa hakika atakuwa amekamilisha daraja zote za dini. Na mwenye kuacha kutafuta hukumu huku kulikotajwa, na asishikamane nako, basi yeye ni kafiri. Na mwenye kuacha pamoja na kushikamana nako, basi ana hukumu ya mfano wake miongoni mwa waasi.