النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعْلَمُ ٱللَّهُ مَا فِى قُلُوبِهِمْ فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَعِظْهُمْ وَقُل لَّهُمْ فِىٓ أَنفُسِهِمْ قَوْلًۢا بَلِيغًا ٦٣
{63} Na ndiyo maana akasema, "Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika nyoyo zao," yani ya unafiki na nia mbaya. "Basi wapuuze." Yani usiwazingatie na wala usiwalipize kwa yale waliyoyafanya na kuyachuma."Na waidhi," yani wabainishie hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kuwahimiza kumfuata Mwenyezi Mungu na kuwahofisha dhidi ya kuiacha. "Na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao." Yani wasihi kwa siri na baina yao. Kwani hilo ndilo la kufanikisha zaidi katika kufikia makusudio, na sisitiza katika kuwakemea na kuwazuia yale waliyo juu yake. Na katika hili kuna ushahidi kuwa mwenye kutenda maasia hata akipewa mgongo, yeye ananasihiwa kwa siri na inasisitizwa katika kumuaidhi kwa yale yanayodhaniwa kufikia makusudio ya hilo.