النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓا۟ إِلَى ٱلطَّـٰغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوٓا۟ أَن يَكْفُرُوا۟ بِهِۦ وَيُرِيدُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًا ٦٠ وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا۟ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ رَأَيْتَ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ٦١
{60 - 61} Mwenyezi Mungu anawashangaza waja wake juu ya hali ya wanafiki ambao wanadai kuwa wanayaamini yale aliyoyaleta Mtume na yale yaliyo kabla yake. Na pamoja na hayo, "wanataka kupeleka kesi yao kwa Twaghut." Naye ni kila mwenye kuhukumu kwa isiyokuwa sheria ya Mwenyezi Mungu. Basi yeye ni Twaghut. Na hali ni kuwa "kwa hakika waliamrishwa kwamba wazikufuru!" Basi vipi linajumuika hili na imani. Maana imani inalazimu kufuata sheria ya Mwenyezi Mungu na kutafuta hukumu yake katika mambo yote. Basi mwenye kudai kuwa yeye ni Muumini, na akaichagua hukumu ya Twaghut badala ya hukumu ya Mwenyezi Mungu, basi yeye ni mwongo katika hilo. Na hili ni katika Shetani kumpoteza, na ndiyo maana akasema, "Na anataka Shetani kwamba awapoteze kupotea kwa mbali" na haki.