النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱبْتَلُوا۟ ٱلْيَتَـٰمَىٰ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغُوا۟ ٱلنِّكَاحَ فَإِنْ ءَانَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَٱدْفَعُوٓا۟ إِلَيْهِمْ أَمْوَٰلَهُمْ ۖ وَلَا تَأْكُلُوهَآ إِسْرَافًا وَبِدَارًا أَن يَكْبَرُوا۟ ۚ وَمَن كَانَ غَنِيًّا فَلْيَسْتَعْفِفْ ۖ وَمَن كَانَ فَقِيرًا فَلْيَأْكُلْ بِٱلْمَعْرُوفِ ۚ فَإِذَا دَفَعْتُمْ إِلَيْهِمْ أَمْوَٰلَهُمْ فَأَشْهِدُوا۟ عَلَيْهِمْ ۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبًا ٦
{6} Al-Ibtilaa ni kumfanyia mtu mtihani na majaribio. Na hilo linakuwa kwa kumpa yatima aliyekaribia kuwa mwenye uamuzi wa busara, ambaye inawezekana afanye uamuzi wa busara kitu kidogo katika mali yake. Na aitumie katika njia inayofaana naye, ili ubainike kwa hilo uamuzi wake wa busara kutokana na upumbavu wake. Na ikiwa ataendelea kutoitumia vizuri, basi hatapewa mali yake. Bali ataendelea kubaki katika upumbavu wake hata akifikia umri mkubwa. Lakini, ukidhihirika uamuzi wake wa busara, na kutengenea kwake katika mali yake, na akafikia umri wa kuoa, "basi wapeni mali zao" kamili na kwa wingi. "Wala msizile kwa kupitiliza," yani, kuvuka mpaka wa halali ambao Mwenyezi Mungu aliwaharamishia katika mali zao. "Na mapema mapema kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima." Yani, wala msizile katika hali ya udogo wao ambayo ndani yake hawawezi kuzichukua kutoka kwao, wala kuwazuia kuzila. Mnaharakisha kufanya hivyo kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima na wazichukue kutoka kwenu, na wawazuie nazo. Na hili ni katika mambo yanayotokea kutoka kwa wengi wa walezi ambao hawana hofu kwa Mwenyezi Mungu wala huruma na upendo kwa mlelewa wao. Wanaiona hali hii kuwa ni hali ya fursa. Kwa hivyo, wanaitumia kama fursa na kuharakisha yale Mwenyezi Mungu aliwaharamishia. Kwa hivyo Yeye Mtukufu akakataza hali hii hasa.