انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النساء
السورة ٤

النساء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٥٠

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا۟ بَيْنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا۟ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا ١٥٠

{150} Hapa kuna makundi mawili ambayo yamebainika kwa kila mtu: Anayemwamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake wote, na Vitabu vyake, na anayekufuru hayo yote. Na limebaki kundi la tatu: nalo ni yule anayedai kuwa anawaamini baadhi ya Mitume na si wengineo, na kwamba hii ni njia ya kumwepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Hakika hili si chochote isipokuwa ni matamanio tu. Kwani hawa wanataka kutofautisha kati ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Kwa maana mwenye kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndiye rafiki kwa hakika, basi atawafanya Mitume wake wote kuwa ndio marafiki wake; kwa sababu hilo ni katika ukamilifu kumfanya kwake kuwa rafiki. Na mwenye kumfanyia uadui yeyote katika Mitume wake; basi kwa hakika atakuwa amemfanyia uadui Mwenyezi Mungu na kuwafanyia uadui Mitume wake wote. Kama alivyosema Yeye Mtukufu "Ambaye ni adui wa Mwenyezi Mungu...} hadi mwisho wa Aya hizi. Na vivyo hivyo mwenye kumkufuru Mtume, basi atakuwa amewakufuru Mitume wote, bali hata yule Mtume ambaye anadai kuwa anamwamini.