النساء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تُجَـٰدِلْ عَنِ ٱلَّذِينَ يَخْتَانُونَ أَنفُسَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمًا ١٠٧
{107} "Wala usiwatetee wale wanaozihini nafsi zao. Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi yule ambaye ni haini mkubwa, mwenye dhambi nyingi.” Hiyana inamaanisha kufanya kosa, na dhulma na dhambi. Na hili linajumuisha kukataza kumbishania yule aliyefanya dhambi na ikamwelekea adhabu kama vile Hadd (adhabu maalumu ya kisheria), au Ta'azir (adhabu ambayo haijakadiriwa kisheria). Basi huyu habishaniwi ili kukana yale aliyofanya ya uhaini au kukanusha yale yanayotokana na hilo ya adhabu ya kisheria. “Hakika, Mwenyezi Mungu hampendi yule ambaye ni haini mkubwa, mwenye dhambi nyingi.” Yani mwingi wa hiana na dhambi. Na ikiwa upendo haupo, basi kinyume chake kinathibiti, ambacho ni chuki. Na hili ni kama sababu ya katazo lililotangulia.