انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الزمر
السورة ٣٩

الزمر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٤

وَأَنِيبُوٓا۟ إِلَىٰ رَبِّكُمْ وَأَسْلِمُوا۟ لَهُۥ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَكُمُ ٱلْعَذَابُ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ٥٤

{54} Lakini kuna sababu za kupata msamaha wake na rehema yake. Ikiwa mja hatazifanya, basi atakuwa amejifungia mlango mkuu na mtukufu zaidi wa rehema na msamaha wake, ambao hakuna sababu yoyote isipokuwa hiyo - yaani, kurejea kwa Mwenyezi Mungu kwa toba ya kweli, kumuomba dua, kunyenyekea, kumfanyia uungu na kumuabudu Yeye tu. Basi njooni kwenye sababu hii tukufu na njia hii kuu zaidi. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu akaamrisha kuharakisha kurejea kwake, akisema: "Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi" kwa nyoyo zenu, "na silimuni kwake." Na katika kauli yake: "Kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake," kuna ushahidi wa kumkusudia Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba bila ya ikhlasi matendo ya nje na ya siri hayafai kitu "kabla ya kukujieni adhabu" kwa njia ambayo haiwezi kuzuilika. "Kisha hapo hamtanusuriwa."