انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ص
السورة ٣٨

ص

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٥

قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ ٦٥

{65} "Sema" ewe Mtume, ukiwaambia hawa wanaokadihibisha, ikiwa watakuomba kisichokuwa chako wala kisichokuwa mkononi mwako: "Hakika mimi ni mwonyaji tu." Huu ndio mwisho wa niliyo nayo, na amri ni ya Mwenyezi Mungu tu. Lakini mimi ninawaamrisha na kuwakataza, na ninawahimiza kutenda mema na kuwakemea dhidi ya maovu. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, basi ni kwa faida yake na mwenye kupotea, basi ni hasara ya nafsi yake. "Na hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu;" yaani, hakuna yule aliye na haki ya kufanyiwa ibada ila Mwenyezi Mungu "Mmoja, Mwenye nguvu zote." Huu ni uthibitisho wa uungu wake kwa ushahidi huu wa kukata, ambao ni upweke wake, Yeye Mtukufu na ushindi wake juu ya kila kitu. Kwani ushindi unalazimu kwamba Yeye ni Mmoja tu. Kwa sababu kamwe haiwezekani kuwepo washindi wawili walio sawa katika ushindi wao. Kwa hivyo, mwenye kushinda kila kitu ndiye wa pekee ambaye,hana aliye sawa naye. Na ndiye anayestahiki kuabudiwa peke yake, kama vile alivyoshinda peke yake.