انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصافات
السورة ٣٧

الصافات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٩٤–٩٦

فَأَقْبَلُوٓا۟ إِلَيْهِ يَزِفُّونَ ٩٤ قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ ٩٥ وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ ٩٦

{94 - 96} "Basi wakamjia upesi upesi" wakitaka kumuadhibu baada ya kuchunguza na wakasema: "Ni nani aliyeifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni katika waliodhulumu." Na wakaambiwa: "Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim," na pia alisema: "Na Wallahi! (Naapa kwa jina la Mweneyzi Mungu) Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya nyinyi mkishageuka kwenda zenu." Basi wakamkemea na kumlaumu, naye akasema: “Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao." Basi waulizeni ikiwa wanaweza kutamka. Basi wakajirudi nafsi zao, wakasema: 'Hakika nyinyi mlikuwa madhalimu!' Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: 'Wewe unajua kwamba hawa hawasemi.' Akasema: 'Basi nyinyi mnawaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, wasiokufaeni kitu wala kukudhuruni...' Hadi mwisho wa aya. Na hapa akasema: "Hivyo mnaviabudu vitu mnavyovichonga wenyewe" kwa mikono yenu na kuviunda? Vipi mnaviabudu ilhali nyinyi ndio mlioviunda, na mnaacha kumkusudia Mwenyezi Mungu "aliyekuumbeni nyinyi na hivyo mnavyovifanya!"