انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصافات
السورة ٣٧

الصافات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٨٥–٨٧

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَاذَا تَعْبُدُونَ ٨٥ أَئِفْكًا ءَالِهَةً دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ ٨٦ فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ٨٧

{85 - 87} Na katika uzima wake ni kwamba ulikuwa mzima (salama) kutokana na kuwadanganya viumbe na kuwahusudia, na maovu mengineyo ya kimaadili. "Alipomwambia baba yake na watu wake: 'Mnaabudu nini?'" Hili ni swali lililokuja kwa mbinu ya kukanusha hayo wanayofanya na kuwafanya wakiri na kuikubali hoja yake. "Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?" Yaani, je, mnaabudu badala ya Mwenyezi Mungu miungu ya uwongo ambayo hata si miungu na isiyofaa kuabudiwa? "Kwani mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?" Kuwa atawafanyia nini nyinyi mnaomuabudu asiyekuwa Yeye? Hili ni tishio kwao kwamba watalipwa adhabu ya kubakia kwa sababu ya kudumu kwao katika ushirikina wao. Na hakika ni upungufu gani mliomdhania Mola Mlezi wa walimwengu ndiyo mkamfanyia wenza na washirika?