الصافات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَعِندَهُمْ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ عِينٌ ٤٨ كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ٤٩
{48 - 49} Alipotaja vyakula vyao, vinywaji vyao, jinsi watakavyokaa, na ujumla wa neema na maelezo yake ya kina kama ilivyo katika kauli yake: "Bustani za neema", aliyabainisha mambo haya kwa kina ili yajulikane ili nafsi ziyatamani. Akawataja wake zao, akasema: "Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha, mazuri." Ima wanawake hawa wana macho ya staha kwa waume zao kwa kuwaelekea wao tu kwa sababu ya usafi wao, na kwa sababu ya uzuri na ukamilifu wa waume wao; kiasi kwamba hawatafuti Peponi yeyote isipokuwa hao, na wala hawatawataka isipokuwa hao tu. Au ni wenye staha kwa sababu waliwafanya waume zao hao kuwaelekea wao tu. Hilo linaonyesha ukamilifu wa uzuri wao mkubwa mno, ambao uliwafanya waume zao kuwatazama wao tu. Kuwatazama kwao waume zao tu pia kunaashiria kwamba wanawapa waume zao hao tu nafsi zao na upendo. Na hizi maana zote mbili zinawezekana, na zote mbili ni sahihi. Yote haya yanaashiria uzuri wa wanaume na wanawake katika Pepo, kupendana kwao wenyewe kwa wenyewe kwa upendo ambao hawawezi kuwatamani wasiokuwa hao, na pia ni ishara ya ukubwa wa ufwasi wao wote, na kwamba humo hakutakuwa na husuda, chuki na kugombana; kwa sababu hakuna sababu za hayo humo. "Wenye macho ya staha mazuri," yenye kufurahisha. "Hao wanawake ni kama mayai yaliyohifadhika" kwa sababu ya uzuri wao, usafi wao, na kwa sababu rangi zao ni rangi bora na nzuri zaidi, ambazo hazina cha kuchukiza wala cha kuwatia dosari.