انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصافات
السورة ٣٧

الصافات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٣٥–٣٦

إِنَّهُمْ كَانُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ ٣٥ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓا۟ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍۭ ٣٦

{35 - 36} Kisha akataja kuwa uhalifu wao ulifikia na hata kuvuka kiwango cha mwisho kabisa. Akasema: "Wao walipokuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu (Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu)" wakalinganiwa kwake, na wakaamrishwa kuacha kuwafanyia uungu wasiokuwa Yeye, "walijivuna" wakiyakataa hayo na wakimpinga yule aliyewajia nayo. Na pia walikuwa "wakisema" kwa njia ya kuyapinga: "Hivyo sisi tuiache miungu yetu" ambayo hatujaacha kuiabudu, sisi na baba zetu, "kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?" Wakimaanisha Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Hawakutosheka - Mwenyezi Mungu awaangamize - na kumpa mgongo na kumkanusha, lakini pia wakamhukumu kwa hukumu yenye dhuluma kubwa zaidi. Akamfanya kuwa mshairi kichaa, na ilhali wanajua kwamba yeye hayajui mashairi wala washairi, wala hasifiki na sifa zao, bali walijua vyema kwamba yeye ndiye mwenye akili zaidi katika viumbe wa Mwenyezi Mungu na mwenye maoni bora zaidi yao wote.