الصافات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلصَّـٰٓفَّـٰتِ صَفًّا ١ فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجْرًا ٢ فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكْرًا ٣ إِنَّ إِلَـٰهَكُمْ لَوَٰحِدٌ ٤
{1 - 4} Hiki ni kiapo chake Mola Mtukufu kuhusu Malaika watukufu katika hali yao ya ibada na usimamizi wao yale wanavyosimamia, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, kwa mujibu wa uungu wake Mwenyezi Mungu aliyetukuka, na umola wake. Akasema: "Ninaapa kwa wanaojipanga kwa safu" katika kumtumikia Mola wao Mlezi, na hao ni Malaika. "Na kwa wenye kukataza mabaya," na wale wanaopeperusha mawingu na mengineyo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. "Na kwa wenye kusoma Ukumbusho," nao ni Malaika wale wanaosoma maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na kwa kuwa wanamfanyia uungu na kumuabudu Mola wao Mlezi, huku wakimtumikia bila ya kumuasi kiasi cha kupepesa jicho. Akaapa kwao kwa uungu wake juu yao, akasema: "Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja," wala hana mshirika yeyote katika uungu. Kwa hivyo mkusudieni Yeye tu kwa upendo wenu, hofu, matumaini, na aina nyinginezo zote za ibada.