انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصافات
السورة ٣٧

الصافات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٨٠–١٨٢

سُبْحَـٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ ١٨٠ وَسَلَـٰمٌ عَلَى ٱلْمُرْسَلِينَ ١٨١ وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ١٨٢

{180 - 182} Alipotaja katika Sura hii maneno yao mengi ya kuchukiza waliyomuelezea nayo, akajiweka mbali nayo, akasema: "Ametakasika Mola wako Mlezi;" yaani Mola Mtukufu "Mola Mwenye enzi" ambaye ni Mwenye nguvu zilizoshinda kila kitu. "Na Salamu juu ya Mitume" kwa sababu wako salama kutokana na madhambi na mapungufu, na pia yako salama yale waliyomsifu nayo Muumba wa ardhi na mbingu. "Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote." Kwa hivyo ni za Mwenyezi Mungu sifa zote njema, kamilifu, zilizo kuu, na vitendo alivyowalea kwavyo walimwengu, akawapa neema nyingi, akawaepusha adhabu mbalimbali, akawaendesha katika harakati zao na utulivu wao na katika hali zao zote. Kwa hivyo Yeye ndiye aliyetakasika mbali na upungufu wowote, anayehimidiwa kwa himidi zote, anayependwa zaidi. Na Mitume wake wako salama na amani iwe juu yao, na yeyote anayewafuata katika hili atapata usalama duniani na akhera, nao maadui zake wataangamia hapa duniani na akhera.

Imekamilika tafsiri ya Surat As-Saffat mnamo Shawwal 6, mwaka wa 1343. Kupitia mikono ya mkusanyaji wake na mwandishi wake, Abdur-Rahman bin Nassir As-Saadi. Na rehema na amani nyingi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mtume wake Muhammad. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye kwa neema zake yanatimia mambo mema.