الصافات
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ ١٢٣ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ ١٢٤ أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ ٱلْخَـٰلِقِينَ ١٢٥ ٱللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ ١٢٦ فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ ١٢٧ إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ ١٢٨ وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ ١٢٩ سَلَـٰمٌ عَلَىٰٓ إِلْ يَاسِينَ ١٣٠ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ ١٣١ إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ ١٣٢
{123 - 132} Mwenyezi Mungu anamsifu mja wake na Mtume wake, Ilyas, rehema na amani ziwe juu yake, kwa unabii, utume na kulinganua kwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba aliwaamrisha watu wake kuwa wachamungu na kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na akawakataza kuabudu sanamu lao liitwalo Baa'li. Aliwakemea kutokana na suala lao la kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu aliyewaumba, akawapa neema za dhahiri na zilizofichika kwa wingi, na akawalaumu: "Vipi mliacha kumuabudu Yule ambaye yuko hivi mkaanza kuabudu sanamu ambalo halidhuru wala halinufaishi, wala haliumbi wala haliruzuku na wala halili chakula wala halizungumzi." Basi je, huu ni nini isipokuwa upotovu mkubwa zaidi, upumbavu na ukengeufu? "Wakamkadhibisha" katika yale aliyowaitia, na wala hawakumtii. Mwenyezi Mungu alisema akiwaahidi adhabu: "Basi kwa hakika watahudhurishwa" Siku ya Kiyama katika adhabu, lakini hapa hakutaja adhabu yao ya duniani, "Isipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa" ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa neema ya kumfuata Nabii wao. Hao hawatahudhurishwa katika adhabu na mateso, bali watapata thawabu nyingi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. "Na tulimwachia (sifa nzuri) kwa waliokuja baadaye." "Iwe salama kwa Ilyas" kutoka kwa Mwenyezi Mungu na waja wake. "Hakika hivyo ndivyo tunavyowalipa waliowema. Hakika yeye ni katika waja wetu walioamini." Hapa Mwenyezi Mungu akawa amemsifu kama alivyowasifu ndugu zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote.