انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الصافات
السورة ٣٧

الصافات

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ ۚ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍۭ ١١

{11} Na alipowabainisha viumbe hawa wakubwa, akasema: "Hebu waulize" hawa wanaokadhibisha uwezekano wa kuumbwa kwao tena baada ya kufa kwao: "Je, wao ndio wenye umbo gumu zaidi?" Yaani, kuwatoa tena baada ya kufa kwao ni kugumu zaidi? "Au hao wengine tuliowaumba," miongoni mwa viumbe hawa? Basi ni lazima watakiri kwamba kuumbwa kwa mbingu na ardhi ndiko kukubwa zaidi kuliko kuumbwa kwa watu. Kwa hilo linawalazimu kukiri kwamba watafufuliwa na kutolewa makaburini. Hata wangerejea nafsini mwao na wakatafakari juu yake, wangetambua kwamba kuanzisha uumbaji wao kutokana na udongo unaonata ni jambo gumu zaidi kulifikiria kuliko kuwaumba tena baada ya kufa kwao. Na ndiyo maana akasema: "Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata," kama vile kauli yake: "Na tulimuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura."