انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يس
السورة ٣٦

يس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٩

وَمَا عَلَّمْنَـٰهُ ٱلشِّعْرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُۥٓ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْءَانٌ مُّبِينٌ ٦٩

{69} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamtakasa Nabii wake Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mbali na walivyomsingizia washirikina kuwa yeye ni mtunzi wa mashairi, na kwamba hayo aliyokuja nayo ni mashairi tu. Akasema: "Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo," kwamba awe mtunga mashairi. Haiwezekani! Kwa sababu yeye ni mwenye hekima, mwongofu, ilhali washairi wamepotea, na wanawafuata wapotevu.Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alivunjilia mbali kila tuhuma ambazo wanazishikilia wale waliopotea mbali na Mtume wake. Alivunjilia mbali uwezekano kwamba yeye ndiye aliyeiandika au kuisoma kutoka kwingine. Kwa hivyo, akajulisha kwamba hakumfundisha ushairi na wala haimfailii kufanya hivyo. "Haukuwa huu ila ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha," ambayo kwayo watu wenye akili watakumbuka matakwa yote ya kidini. Kwani inajumuisha hayo yote kwa njia kamilifu zaidi. Na inazikumbusha akili juu ya yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka katika maumbile yao ya asili ya kuamrisha kila jema, na kukataza kila ovu. "Qur-ani inayobainisha" yale yanayohitajika kubainishwa. Na ndiyo maana akafuta kinachobainishwa ili hilo lionyeshe kwamba inabainisha haki yote kwa ushahidi wake wa kina na wa jumla, na pia inabainisha batili na ushahidi wa ubatilifu wake. Mwenyezi Mungu aliiteremsha hivyo kwa Mtume wake.