يس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَوْ نَشَآءُ لَمَسَخْنَـٰهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ ٦٧
{67} "Na tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi" nyuma, ili wawe mbali na Moto. Maana yake ni kwamba hawa makafiri lilikwisha wadhibitikia neno la adhabu, na ikabidi waadhibiwe. Na mahali hapo hapatakuwa isipokuwa Moto uliodhihirishwa, ambao hakuna atakayeweza kuokoa isipokuwa kwa kuvuka kupitia juu Sirat (njia iliyoko juu ya Moto), jambo ambalo hawaliwezi isipokuwa watu wa imani ambao wanatembelea katika nuru yao. Ama hawa, hawana agano lolote kwa Mwenyezi Mungu kwamba wataokoka kutokana na Moto. Akitaka, atayafutilia mbali macho yao na akaacha watembee, kwa hivyo wasiweze kuifikia Njia iliyonyooka hata kama wataiwania na kuikimbilia. Na akitaka, anaondoa harakati zao, kwa hivyo wasiweze kwenda mbele wala nyuma. Na maana ya haya ni kwamba hawakuweza kuivuka njia hiyo, kwa hivyo, kamwe hawataokoka.