يس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمْ فَهُمْ غَـٰفِلُونَ ٦
{6} Mwenyezi Mungu alipoapa kwa ujumbe wake, na kuuthibitisha kwa ushahidi mbalimbali, akataja haja kubwa ya viumbe juu yake, akasema: "Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika." Ambao ni wale Waarabu wasiojua kusoma na kuandika, ambao bado hawakuwa na vitabu na Mitume, ambao walikuwa wamejumuishwa na ujinga na kugubikwa na upotofu, na akili za walimwengu zikawacheka kwa upumbavu wao. Basi Mwenyezi Mungu akawatumia Mtume kutokana nao wenyewe, ili awatakase na awafundishe Kitabu na hekima, ijapokuwa kabla ya hapo walikuwa katika upotofu uliowazi. Alipaswa kuwaonya Waarabu wasiojua kusoma na kuandika na watu wote wanaofanana nao miongoni mwa wale wasiojua kusoma na kuandika, na awakumbushe Watu wa Kitabu vitabu walivyo navyo. Kwa hivyo, Mtume huyu akawa ni neema ya Mwenyezi Mungu juu ya Waarabu hasa na juu ya watu wengine kwa ujumla.