يس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ ٱلْيَوْمَ فِى شُغُلٍ فَـٰكِهُونَ ٥٥ هُمْ وَأَزْوَٰجُهُمْ فِى ظِلَـٰلٍ عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ ٥٦
{55 - 56} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kwamba kila mtu hatalipwa ila kwa aliyoyatenda,akataja malipo ya makundi hayo mawili, na akaanza na malipo ya watu wa Peponi. Akajulisha kwamba siku hiyo watakuwa “shughulini, wamefurahi" kwa sababu ya kila kitu ambacho nafsi inakitamani, na macho yanakipenda, na yale yanayotamaniwa na wanaoyatamani, na hayo ni pamoja na kuingiliana na wanawali warembo. Kama alivyosema: "Wao na wake zao" miongoni mwa hurulaini waliojumuisha kati ya nyuso na miili mizuri na maadili bora "wamo katika vivuli juu ya viti vya fahari" vilivyopambwa kwa mavazi mazuri ya urembo, "wameegemea" juu yake kuegemea kunakoashiria raha kamili, utulivu na ladha.