انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يس
السورة ٣٦

يس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢

إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا۟ وَءَاثَـٰرَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ فِىٓ إِمَامٍ مُّبِينٍ ١٢

{12} "Hakika Sisi tunawafufua wafu" ili tuwalipe kwa matendo yao. Na tunayaandika wanayoyatanguliza miongoni mwa mambo mema na maovu waliyotenda katika uhai wao, "na wanayoyaacha nyuma" ambazo ni athari za heri na athari za shari ambazo walikuwa wao ndio sababu ya kutokea kwake wakati wa uhai wao na baada ya kufa kwao. Na vile vitendo vilivyotokana na maneno yao, vitendo vyao na hali zao. Kila heri aliyofanya mtu kwa sababu ya elimu aliyochukua kwa mtu fulani, au aliyomfundisha, au nasaha, kumuamrisha mema, au kumkataza maovu, au elimu aliyofunza wanafunzi au aliyoandika katika vitabu vyenye kunufaisha wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake. Au akafanya heri kama vile swala, zaka, sadaka, au ihsani, kwa hivyo wengine wakamuiga, au alijenga msikiti au mahali ambapo watu wanakaa na mengineyo; basi hayo yote ni katika athari zake ambazo ameandikiwa, pamoja na matendo yake maovu. Ndiyo maana Nabii, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema: “Mwenye kuanzisha mwenendo mwema atapata ujira wake na ujira wa mwenye kuutenda mpaka Siku ya Kiyama. Na mwenye kuanzisha mwenendo muovu, basi mzigo wake uko juu yake, na mzigo wa mwenye kuutenda mpaka Siku ya Kiyama." Sehemu hii inakuonyesha kiwango cha juu cha kulingania kwa Mwenyezi Mungu na kuongoka kufikia njia yake kwa kila njia inayofikisha kwenye hilo, na kiwango cha chini cha kiongozi wa kulingania kwenye uovu. Na kwamba yeye ndiye kiumbe wa chini kabisa, na mkubwa wao zaidi katika uhalifu, na mwenye madhambi kubwa zaidi yao wote. "Na kila kitu" miongoni mwa matendo, makusudio na mambo mengineyo "tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha." Yaani, Kitabu ambacho ni mama wa vitabu vyote, na kwake ndiyo marejeo ya vitabu vilivyo mikononi mwa Malaika, nacho ndio Ubao Uliohifadhiwa.