انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · فاطر
السورة ٣٥

فاطر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَىٰ حِمْلِهَا لَا يُحْمَلْ مِنْهُ شَىْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰٓ ۗ إِنَّمَا تُنذِرُ ٱلَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِٱلْغَيْبِ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ ۚ وَمَن تَزَكَّىٰ فَإِنَّمَا يَتَزَكَّىٰ لِنَفْسِهِۦ ۚ وَإِلَى ٱللَّهِ ٱلْمَصِيرُ ١٨

{18} Maana ya mwisho inaashiriwa na aliyoyataja baada yake katika kauli yake: "Na mbebaji hatabeba mzigo wa mwengine" Siku ya Kiyama. Kila mmoja atalipwa kwa matendo yake, na hakuna atakayebeba dhambi ya mwengine. "Na aliyetopewa na mzigo wake" yaani, nafsi iliyolemewa na madhambi ikitafuta msaada ili isaidiwe kuibeba baadhi ya mizigo yake "hautachukuliwa hata kidogo, hata kama ni jamaa yake." Kwa sababu hali ya Akhera si kama hali ya dunia ambapo rafiki alikuwa akimsaidia rafiki yake. Bali Siku ya Kiyama mja atatamani lau angekuwa na haki juu ya yeyote, hata kama ni juu ya wazazi wake na jamaa zake. "Hakika wewe unawaonya wale wanaomcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Swala." Yaani, hawa ndio wanaokubali maonyo, na kunufaika nayo, watu wanaomcha Mwenyezi Mungu kwa ghaibu. Wale wanaomuogopa kwa siri na hadharani, wanaosimamisha Swala kwa mipaka yake, masharti yake, nguzo zake, wajibu wake na unyenyekevu wake. Kwa sababu kumhofu Mwenyezi Mungu kunamtaka mja kufanya yale ambayo anayahofia kwamba asipoyafanya ataadhibiwa. Nayo swala inaitia mema na inakataza machafu na maovu. "Na mwenye kujitakasa" kwa kujiweka mbali na kasoro kama vile unafiki, kujionyesha, kiburi, uwongo, udanganyifu, hadaa, njama mbaya na maadili mengine mabaya, na akawa na maadili mazuri kama vile ukweli, ikhlasi, unyenyekevu, ulaini kwa watu (upole) na nasaha nzuri kwa waja wake, na kifua chake kikawa salama kutokana na chuki, husuda, na maadili mengine maovu; basi manufaa ya kujitakasa kwake huku yanamrudia mwenyewe na madhumuni yake yatamfikia yeye, na hakuna chochote katika matendo yake yatayopotea. "Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu." Naye atawalipa viumbe kwa yale waliyofanya kabla, na atawafanyia hesabu kwa yale waliyoyatanguliza, na wala hataacha kitu chochote kidogo wala kikubwa isipokuwa atakihesabu.