الروم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱللَّهُ يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ١١ وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُبْلِسُ ٱلْمُجْرِمُونَ ١٢ وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَآئِهِمْ شُفَعَـٰٓؤُا۟ وَكَانُوا۟ بِشُرَكَآئِهِمْ كَـٰفِرِينَ ١٣
{11 - 13} Mwenyezi Mungu anatujulisha kwamba Yeye ndiye pekee anayeanzisha uumbaji wa viumbe, kisha akavirudisha. Kisha kwake watarejeshwa baada ya kurudishwa kwao, ili awalipe kwa vitendo vyao. Ndiyo maana akataja malipo ya watu waovu, kisha malipo ya watu wema. Akasema, "Na siku itakaposimama Saa ya Kiyama," na watu wasimame mbele ya Mola Mlezi wa walimwengu wote [na wakione] Kiyama kwa macho yao wenyewe, siku hiyo "wahalifu watakata tamaa" juu ya kila heri, na hilo ni kwa sababu hawakuitangulizia siku hiyo isipokuwa uhalifu, ambao ni madhambi kama vile ukafiri, ushirikina na maasi. Kwa hivyo, walipotanguliza sababu za adhabu, na hawakuzichanganya na chochote katika sababu za kulipwa mazuri, wakakata tamaa, wakafilisika, na yakawapotea yale waliyokuwa wakiyazua ya kunufaishwa na washirika wao, na kwamba watawafanyia uombezi. Ndiyo maana akasema, "Wala hawatakuwa na waombezi wowote miongoni mwa wale waliokuwa wakiwashirikisha na Mwenyezi Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao." Hao washirikina watajitenga mbali na wale ambao wao wenyewe waliwashirikisha pamoja na Mwenyezi Mungu, na pia wale walioabudiwa watajitenga nao, na watasema: Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi.