انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · القصص
السورة ٢٨

القصص

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ ٤

{4} Basi mwanzo wa kisa hiki ni kwamba "Hakika Firauni alitakabari katika ardhi" katika ufalme wake, mamlaka yake, askari wake, na nguvu zake, na akawa katika wanaotakabari katika hayo, na si katika walio juu ndani yake, "na akawagawa wananchi makundi mbalimbali" akawa anawafanyia kulingana na matamanio yake na kutekeleza ndani yao kile anachotaka kama vile kuwashinda na kuwakandamiza. "Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao," na taifa hilo ni Wana wa Israili, ambao Mwenyezi Mungu aliwaboresha juu ya walimwengu, jambo ambalo lingempasa kuwatukuza na kuwaheshimu, lakini aliwadhoofisha kwa sababu aliona kwamba hawana kizuizi cha kumzuia kufanya anachowatakia. Kwa hivyo akawa hawajali wala kujali mambo yao, na akafikia hali kwamba alikuwa "akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha hai watoto wao wanawake," akihofia kwamba wataongezeka katika nchi yake, na wauchukue ufalme huo. "Hakika yeye alikuwa katika waharibifu," ambao hawana nia yoyote katika kufanya mambo ya dini kutengenea wala mambo ya dunia. Na hili ni katika kufanya kwake uharibifu katika dunia.