النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَقَدْ وُعِدْنَا هَـٰذَا نَحْنُ وَءَابَآؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ ٦٨
{68} "Hakika ni haya haya tu tuliahidiwa" yaani, ufufuo "sisi na baba zetu zamani" yaani, hayakutujia wala hatukuona chochote katika hayo. "Hayakuwa haya isipokuwa ni hadithi za uongo za watu wa kale." Yaani, hadithi zao na habari ambazo wanapitisha tu nyakati kwazo, wala hazina msingi wowote, wala ukweli wowote ndani yake. Kisha akahama akaacha kujulisha juu ya hali za wale wanaokadhibisha na akaanza kujulisha kwamba hawajui wakati wa kuja kwa Akhera, kisha kujulisha juu ya udhaifu wa elimu yao ndani kuhusiana na hilo, kisha kujulisha kwamba ni shaka tu, kisha kujulisha kwamba ni upofu, kisha kujulisha juu ya kulikataa kwao hilo na kuona kwao kwamba haliwezi kutokea. Basi ndiyo maana hofu ikaondoka mioyoni mwao, kwa hivyo wakaelekea katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na ikawawia rahisi kukadhibisha haki, na kusadiki batili, na wakahalalisha matamanio yao na wakaacha kufanya ibada, kwa hivyo wakahasiri dunia yao na Akhera yao.