النمل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلَـٰمٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ ٱلَّذِينَ ٱصْطَفَىٰٓ ۗ ءَآللَّهُ خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ ٥٩
{59} Yaani, sema sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye anastahili ukamilifu wa kuhimidiwa, sifa, na kutajwa kwa uzuri, kwa sababu ya ukamilifu wa sifa zake, na uzuri wa wema wake, na zawadi zake, na uadilifu wake na hekima yake katika kuwaadhibu kwake wale wanaokadhibisha, na kuwatesa madhalimu, na pia aliwapa salama waja wake ambao aliwateua na kuwachagua juu ya walimwengu miongoni mwa manabii na mitume na watu wa hadhi ya juu zaidi kwa Mwenyezi Mungu, Mola mlezi wa walimwengu. Na hilo ni kwa ajili ya kuinua utajo wao na kuashiria cheo chao na usalama wao kutokana na uovu na uchafu, na usalama wa kile walichosema kuhusiana na Mola wao Mlezi kutokana na mapungufu na kasoro. "Je, Mwenyezi Mungu ndiye bora, au wale wanaowashirikisha naye?" Na hili ni swali ambalo linajulikana vyema sana. Yaani, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi, Mkuu, Mwenye sifa kamilifu, mwenye upole mkubwa ndiye bora au masanamu na vyote vinavyoabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu ilhali hivyo ni vipungufu kwa njia zote; havinufaishi wala havidhuru, wala havijimilikii vyenyewe wala wale wanaoviabudu uzito wa chembe ya wema. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu ndiye mbora kuliko hao wanaowashirikisha naye.