انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٢

وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِى جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَآءَ مِنْ غَيْرِ سُوٓءٍ ۖ فِى تِسْعِ ءَايَـٰتٍ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَقَوْمِهِۦٓ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ ١٢

{12} "Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi" bila ya kuwa na ukoma wala upungufu, lakini badala yake utakuwa na weupe wa kushangaza mwenye kutazama miale yake. "Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake." Yaani, ishara mbili hizi - kugeuka kwa fimbo kuwa nyoka anayekwenda mbio, na kuutoa mkono kutoka mfukoni hali ya kuwa ni mweupe - ni miongoni mwa ishara tisa ambazo utakwenda nazo na kumlingania kwazo Firauni na watu wake. "Hakika hao walikuwa kaumu waovu." Walitoka katika mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa ushirikina wao na kupanda kwao vichwa, na kujiinua kwao juu ya waja wa Mwenyezi Mungu na kutakabari kwao katika ardhi bila ya haki.