انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠

وَأَلْقِ عَصَاكَ ۚ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَـٰمُوسَىٰ لَا تَخَفْ إِنِّى لَا يَخَافُ لَدَىَّ ٱلْمُرْسَلُونَ ١٠

{10} "Na itupe fimbo yako!" Kwa hivyo, akaitupa, "alipoiona ikitikisika kama nyoka" wa kiume mwenye kwenda haraka; "aligeuka nyuma wala hakungoja," kwa sababu ya kumuogopa nyoka huyo ambaye alimwona kulingana na maumbile ya asili ya mwanadamu. Mwenyezi Mungu akamwambia: "Ewe Musa! Usihofu!" Na akasema katika aya nyingine: "Njoo mbele wala usiogope. Hakika wewe ni miongoni mwa waliosalimika." "Hakika hawahofu mbele yangu Mitume." Kwa sababu hofu zote zimejumuishwa katika majaliwa yake, uendeshaji wake, na amri, yake. Kwa hivyo, wale ambao Mwenyezi Mungu aliwachagua kwa ajili ya utume na akawateua kwa ajili ya ufunuo wake, hawapaswi kumwogopa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, haswa wakati wanapokuwa karibu zaidi naye, na kuwa na fursa ya kuongeleshwa naye.