انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النمل
السورة ٢٧

النمل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١

طسٓ ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْقُرْءَانِ وَكِتَابٍ مُّبِينٍ ١

Mwenyezi Mtungu Mtukufu anawatabahisha waja wake juu ya ukuu wa Qur-ani, na anaashiria kwake kwa ishara ya kuitukuza. Alisema, "Hizi ni Aya za Qur-ani na Kitabu kinachobainisha." Yaani, ndizo ishara za juu zaidi, na ushahidi wenye nguvu zaidi, na dalili za wazi zaidi na zenye kubainisha zaidi matashi makubwa zaidi na mambo bora zaidi yatafutwayo, na matendo bora zaidi, na tabia safi zaidi. Ni Aya zinazoonyesha habari za ukweli, na amri nzuri, na makatazo ya kila tendo baya na tabia ya kukashifiwa. Ni aya ambazo zilifikia katika uwazi wake na kuabinisha kwake hoja zinazong'aa kiwango ambacho jua linafikia kwa macho. Ni aya ambayo zilionyesha imani, na ziliitia kufikia yakini, na zikajulisha juu ya ghaibu zilizopita na zijazo kama zilivyokuwa na kama zikatakavyokua kihalisia. Ni aya zilizoitia kujua Mola Mlezi, Mkuu kwa majina yake mazuri zaidi, na sifa zake za juu zaidi, na matendo yake kamili. Ni aya ambazo zilitujulisha kuhusu Mitume wake, vipenzi wake, na zikawaelezea mpaka ikawa ni kama kwamba tunawaangalia kwa macho yetu.