الشعراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ءَايَةً فَظَلَّتْ أَعْنَـٰقُهُمْ لَهَا خَـٰضِعِينَ ٤
{4} Na ndiyo sababu akasema, "Tungependa, tungeliwateremshia kutoka mbinguni Ishara," miongoni mwa ishara hizo wanazozipendekeza wao, "zikashinda shingo zao" yaani wakadhibishao hao "zimezinyenyekea." Lakini hakuna haja yoyote wala masilahi ya kufanya hilo. Kwa maana wakati huo imani itakuwa haina manufaa yoyote. Kwa sababu imani yenye manufaa ni kuamini ghaibu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Je, wanangoja jingine isipokuwa wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapofika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu..." hadi mwisho wa Aya.