الشعراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَـٰتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ ٣٨ وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ ٣٩ لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ ٱلسَّحَرَةَ إِن كَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ ٤٠
{38-40} Kwa hivyo Firauni akafanya kulingana na maoni yao, na akatuma mijini wenye kukusanya wachawi, na akafanya bidii kubwa sana katika hilo. "Basi wakakusanywa wachawi kwa ajili ya miadi ya siku maalumu," ambayo Musa aliwaahidi. Nayo ilikuwa siku ya mapambo ambayo hawafanyi kazi ndani yake. "Na watu wakaambiwa: Je, mtakusanyika" katika siku hiyo mliyoahidiwa? "Huenda tutawafuata wachawi ikiwa wao ndio watakaoshinda." Kwa maana wao ni mahiri katika tasnia zao, kisha tuwafuate na kuwatukuza na kutambua ubora wa elimu ya uchawi. Na lau kama wangelifanikiwa kufikia haki, basi wangesema: Huenda tumfuate mwenye haki na tujue lililo sahihi. Na ndiyo maana, halikuwanufaisha hilo isipokuwa tu kuwasimamishia hoja.