انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الشعراء
السورة ٢٦

الشعراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٣٤–٣٧

قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُۥٓ إِنَّ هَـٰذَا لَسَـٰحِرٌ عَلِيمٌ ٣٤ يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِۦ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ ٣٥ قَالُوٓا۟ أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَٱبْعَثْ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَـٰشِرِينَ ٣٦ يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ ٣٧

{34-37} (Firauni) akawaambia waheshimiwa waliomzunguka akipinga haki na yule aliyekuja nayo. "Hakika huyu ni mchawi mtaalamu." "Anataka kuwatoa katika nchi yenu." Aliwaficha ukweli kwa sababu alijua kwamba wana udhaifu wa akili, kwamba hili ni katika yale ambayo wachawi hufanya, kwa sababu wao walikuwa wanajua kwamba wachawi wanafanya maajabu ambayo watu hawawezi kufanya, na akawahofisha kwamba makusudio yake kwa uchawi huu ni kuutumia kuwatoa katika nchi yao, ili wang'ang'ane na kufanya bidii ya kumpinga yeyote anayetaka kuwaondoa kwa watoto wao na nyumba zao. "Basi mna shauri gani?" "Wakasema: Mpe muda yeye na kakaye na uwatume mijini wakusanyao watu;" ili hao wakusanyaji "Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu." Kwa maana, mchawi anakabiliwa na uchawi wa aina sawa na uchawi wake. Na hili ni katika wema wa Mwenyezi Mungu; kwamba awaonyeshe waja wake ubatili wa yale ambayo aliyowaficha watu Firauni mjinga mpotovu mpotezaje kwamba kile alicholeta Musa ni uchawi. Kwa hivyo, aliwafanya kukusanya watu wa ujuzi katika uchawi; ili kikao hicho kiwe mbele ya viumbe wengi, ili haki ishinde batili, na ili wenye elimu na wana tasnia hii wakubali usahihi wa kile alicholeta Musa, na kwamba huo si uchawi.