انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الفرقان
السورة ٢٥

الفرقان

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٠

إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَـٰلِحًا فَأُو۟لَـٰٓئِكَ يُبَدِّلُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِهِمْ حَسَنَـٰتٍ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ٧٠

{70} "Isipokuwa atakayetubu" akaacha dhambi hizi na mengineyo mara moja, na akajuta kwa yale aliyofanya katika hayo, na akaazimia azimio la uhakika kwamba hatarudia. "Na akaamini" Mwenyezi Mungu sahihi yenye kulazimu kuacha dhambi na kufanya utii. "Na akatenda matendo mema" miongoni mwa yale ambayo Mwenye sheria aliamrisha kufanya ikiwa atakusudia kwayo uso wa Mwenyezi Mungu. "Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mazuri;" yaani, vitabadilishwa vitendo vyao na maneno yao ambayo yalikuwa tayari kufanya mabaya yawe mazuri. Kwa hivyo, ushirikina wao ukabadilika ukawa imani, na maasia yao yakawa utii, na yanabadilika mabaya yao yenyewe waliyoyafanya, kisha wakatubia kila dhambi, na wakarudi kwa Mwenyezi Mungu, na wakatii, hayo yote yanabadilika yawe matendo mazuri, kama ilivyo dhahiri katika aya hii, na pia ilisimuliwa kuhusiana na hilo hadithi ya mwanamume ambaye Mwenyezi Mungu alimfanyia hesabu juu ya baadhi ya dhambi zake, na kisha akabadilisha mahali pa kila baya kuwa zuri. Kwa hivyo akasema, "Ewe Mola Mlezi! Hakika, nina mabaya mengine ambayo siyaoni hapa. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe." kwa anayetubia, Yeye husamehe dhambi kubwa. "Mwingi wa kurehemu" waja wake, ambapo aliwaita kutubu baada ya kufanya waziwazi madhambi makuu, kisha akawawezesha kutubia, kisha akaikubali kutoka kwao.