انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الفرقان
السورة ٢٥

الفرقان

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢١

وَقَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْنَا ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَوْ نَرَىٰ رَبَّنَا ۗ لَقَدِ ٱسْتَكْبَرُوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِمْ وَعَتَوْ عُتُوًّا كَبِيرًا ٢١

{21} Yaani, walisema wale waliokadhibisha Mtume, waliokadhibisha ahadi nzuri na ahadi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu, ambao mioyoni mwao hakuna hofu ya ahadi ya adhabu hiyo wala matumaini ya kukutana na Muumba: "Mbona sisi hatukuteremshiwa Malaika au tumwone nasi Mola wetu Mlezi?" Yaani, kwa nini Malaika hawangeshuka ili wakushuhudilie wewe huo ujumbe wako na wakuunge mkono juu yake, au washuke tu kama mitume kivyao, au tumwone Mola wetu Mlezi, ili atusemeshe akisema, "Huyu ni Mtume wangu. Basi mfuateni yeye!" Na huku ni kumpinga Mtume kwa kile kisichofaa hata kuwa pingamizi, lakini ni kwa sababu ya kutakabari, kiburi, na kuvuka mipaka. "Hakika, hawa wamejiona bora nafsi zao," kwa maana walipendekeza pendekezo hili na kuthubutu kwa ujasiri huu. Basi nyinyi ni nani enyi mafukara, maskini hadi mkaomba kumwona Mwenyezi Mungu na mkadai kwamba, kuukubali ujumbe wake kunategemea tu juu ya kuthibiti hilo? Na ni kiburi gani kikubwa zaidi kuliko hiki? "Na wamepanda kichwa, vikubwa mno!" Yaani, wamekuwa wagumu na kukakamia kuikataa haki ugumu mkubwa mno, kwa hivyo mioyo yao ni migumu zaidi kuliko mawe na ni imara zaidi kuliko chuma, hailainiki kwa sababu ya ukweli wala haiwasikilizi washauri. Na ndiyo maana hawakuingiwa mawaidha wala ukumbusho, wala hawakufuata haki wakati mwonyaji alipowajia, bali walikabiliana na mkweli zaidi wa viumbe wote na ishara za Mwenyezi Mungu zilizo wazi, kwa kuzipa mgongo na kuzikadhibisha [na kuzipinga]. Basi ni kupanda kichwa kupi kukubwa kuliko huku? Na ndiyo maana, matendo yao yalibatilika, na kupotelea mbali, na wakahasirika hasara kubwa mno, [na wakanyimwa kunyimwa kukubwa zaidi].