انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النور
السورة ٢٤

النور

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٨–٩

وَيَدْرَؤُا۟ عَنْهَا ٱلْعَذَابَ أَن تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَـٰدَٰتٍۭ بِٱللَّهِ ۙ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ ٨ وَٱلْخَـٰمِسَةَ أَنَّ غَضَبَ ٱللَّهِ عَلَيْهَآ إِن كَانَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ ٩

{8-9} "Na mke itamwondokea adhabu." Yaani, adhabu itamwondokea ikiwa atakabiliana na shuhuda za mume wake kwa shuhuda za aina yake zinazofanana na hizo; "kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba, mume huyu ni miongoni mwa waongo," na akaongeza sehemu ya tano, akithibitisha na kusisitiza hilo kwa kujiombezea hasira za Mwenyezi Mungu juu yake. Basi ikitimia laana kati yao; hutenganishwa baina yao "hadi" milele, na hutolewa na kukataliwa mtoto ambaye atapakitana katika laana hii kwake yeye. Yaani, baada ya mke na mume kuchukua laana, na ikawa mke yule ana uja uzito. Basi mtoto atakayemzaa hataakuwa wa mume huyo aliyemlaani. Maana ya wazi ya Aya inajuulisha kushurutishwa maneno haya wakati wa kulaani kutoka kwake mume au mke. Na imeshurutishwa kuwekewa utaratibu na mpangilio maalamu ndani yake, na kwamba hakuna kitu kitakachopunguzwa kutoka kwa utaratibu huo, na hakuna kitu kinachopaswa kubadilishwa na chochote. Na kwamba, laana ni maalumu na mahususi kwa mume ikiwa atamtuhumu mkewe, si kinyume chake. Na kwamba kumfananisha mtoto kwa aliyelaaniwa hakuna uzingatifu kwalo. Kama vile haizingatiwi kulala kwao pamoja, na huzingatiwa mfanano ikiwa hakuna anayependekezwa zaidi isipokuwa yeye mume.