النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُوا۟ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٥
{5} Na kauli yake, "Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengenea - hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." Kutubia katika sehemu hii, ni kwa yule mchochezi aliyeikadhibisha nafsi yake yeye mwenyewe, na kukiri kwamba yeye ni mwongo katika yale aliyoyasema. Na ni wajibu ajikanushe nafsi yake, hata akiwa na yakini kwa kutokea kwake; ambapo hakuleta mashahidi wanne. Ikiwa mchochezi atatubia, akarekebisha amali yake ikawa njema, na akabadilisha ubaya wake kwa vitendo vizuri. Upotovu umeondolewa kwake, na ushahidi wake unakubaliwa kuwa ni sahihi. "Kwani bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu." Anasamehe madhambi yote kwa wanaotubu na kujikurubisha kwake yeye. Bila shaka mchochezi atapigwa ikiwa hataleta mashahidi wanne na ikiwa si mume katika ndoa yake, na ikiwa ni mume, basi ametajwa kwa kauli yake