انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النور
السورة ٢٤

النور

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٦

لَّقَدْ أَنزَلْنَآ ءَايَـٰتٍ مُّبَيِّنَـٰتٍ ۚ وَٱللَّهُ يَهْدِى مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ ٤٦

{46} Yaani: tumewarehemu waja wetu na tukawateremshia Aya zilizo wazi; yaani, ushahidi ulio wazi wa malengo yote ya halali, adabu zinazosifiwa, na elimu ya busara. Hivyo, njia zikadhihirika, na uwongofu ukadhihirika kutokana na upotofu na uongofu kutokamana na upotofu. Hakuna tuhuma hata kidogo iliyobaki kwa yeyote ambaye ni mwongo kuhusu hilo, wala tatizo dogo kwa wale wanaotaka kufanya lililo sawa. Kwa sababu ni wahyi utokao kwa yule ambaye ujuzi wake ni mkamilifu, ambaye rehema yake ni kamilifu, na maelezo yake ni kamili. Hakuna maelezo baada ya kauli yake. Baada ya hayo, mwenye kuangamia ataangamia kwa dalili zilizo wazi, na atakayeishi ataishi na ushahidi ulio wazi. ''Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye,'' miongoni mwa waliotangulia mbele ya wema na uwongofu; ''katika njia iliyonyooka;'' yaani, njia iliyo wazi, fupi inayomfikisha kwake na kwenye jumba la utukufu wake, ikiwa ni pamoja na elimu ya haki, kuipendelea, na kuifanyia kazi. Alisambaza taarifa kamili ya uumbaji wote, na akaufanya uwongofu wake mahsusi kwa amtakaye. Hii ni fadhila yake na hisani, na ni ipi fadhila ya Mwingi wa kushukuru kwa mwenye kumshukuru? Huo ndio uadilifu wake, na huvunja hoja kwa mwenye kutoa hoja. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi pa kuiweka pamoja na sehemu za hisani yake.