انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النور
السورة ٢٤

النور

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٩

لَّيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَدْخُلُوا۟ بُيُوتًا غَيْرَ مَسْكُونَةٍ فِيهَا مَتَـٰعٌ لَّكُمْ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا تَكْتُمُونَ ٢٩

{29} Hukumu hii inatumika kwa nyumba zinazokaliwa iwe ndani yake kuna vitu vya mtu au la, na katika nyumba zisizo na watu ambazo ndani yake hakuna vitu vya mtu. Ama kuhusu nyumba ambazo hazina wakaaji ndani yake, na kuna vitu vya mtu anavyohitaji kuviingia, na hakuna awezaye kumuomba ruhusa ndani yake, na haya ni kama katika nyumba za kupanga na nyinginezo, hakika ameyataja kwa kusema, "Si vibaya kwenu." Yaani, si kosa wala dhambi. Hii inaashiria kuwa kuingia katika majumba yaliyotangulia bila ya kuomba ruhusa ni haramu na ndani yake kuna makosa "Kuingia nyumba zisizokaliwa, ambazo ndani yake yamo manufaa yenu." Hii ni katika tahadhari ya ajabu ya Qur-an, kwani hakika kauli yake, "Msiingie nyumba zisizokuwa zenu," ni kauli ya jumla katika kila nyumba isiyo miliki ya mtu. Mwenyezi Mungu Mtukufu alizitoa humo nyumba zisizokuwa miliki yake na ndani yake muna vitu vyake na hazikuwa na mkaaji ndani yake. Likaondoka kosa na dhambi la kuingia ndani yake bila ruhusa. "Na Mwenyezi Mungu anajua mnayoyadhihirisha na mnayoyaficha." Hali zenu zilizo dhahiri na zilizofichikana, na kujua maslahi yenu. Kwa hivyo amewaandikia sheria mnayohitaji na mnalazimishwa kufanya kutokana na hukumu za kisheria.