النور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ ٱلْفَـٰحِشَةُ فِى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ١٩
{19} "Kwa hakika wale wanaopenda uenee uchafu." Yaani, mambo machafu na ya kuchukiza, na wanapenda machafu yajulikane "kwa walioamini, watapata adhabu chungu." Yaani, yenye maumivu ya moyo na mwili, na hiyo ni kwa sababu aliwahadaa ndugu zake Waislamu; na mapenzi yake ya uovu kwao, na ushupavu wake katika kuwapinga kwao. Ikiwa tishio hili lilikuwa tu kwa sababu ya kupenda maovu na mabaya kuenea, na kuufanya kuwa halali moyoni; basi vipi kuhusu jambo kubwa kuliko hilo, kama vile kuudhihirisha uovu huo na kuusambaza? Sawa uwe uchafu ulifanyika au haukufanyika, yote haya yanatokana na rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waaminifu, na ulinzi wa kuhufadhi heshima yao. Kama alivyolinda damu zao na mali zao, na akawaamrisha kufanya yale yanayohitaji usawa kati yao, na kwamba kila mmoja wao ampende ndugu yake anachokipendelea nafsi yake, na achukie kwa ajili yake anachokichukia nafsi yake. "Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui." Na kwa hivyo, akawafundisha, na akakwabainishieni msiyoyajua.