المؤمنون
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِيَنِّى مَا يُوعَدُونَ ٩٣ رَبِّ فَلَا تَجْعَلْنِى فِى ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ ٩٤ وَإِنَّا عَلَىٰٓ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمْ لَقَـٰدِرُونَ ٩٥
{93-95} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoweka ushahidi wake mkubwa dhidi ya wakanushaji, hawakuizingatia, wala hawakuinyenyekea, adhabu ilistahiki juu yao, na wakaahidiwa kuwa itashuka, na Mwenyezi Mungu akamwongoza Mwenyezi Mungu mtume wake aseme: "Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa;" yaani, wakati wowote utakaponionyesha adhabu yao na unitahadharishe mimi juu ya hilo, "Mola wangu Mlezi! Usinijalie katika watu madhalimu hao;" yaani, nikinge mimi na unirehemu kutokana na utakayowapa shida kwayo kutokana na dhambi zinazowajibisha kisasi, na unilinde vile vile kutokana na adhabu itakayowashukia ; kwa sababu adhabu huenea wakati wa kushuka kwake kwa aliyeasi na mwenginewe. Amesema Mwenyezi Mungu katika kukaribia kwa adhabu yao: "Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyesha tuliyowaahidi," na lakini tukichelewesha;ni kwa hekima; la sivyo; uweza wetu unaswihisha kutokea adhabu hii "juu yao."