المؤمنون
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
بَلْ قَالُوا۟ مِثْلَ مَا قَالَ ٱلْأَوَّلُونَ ٨١ قَالُوٓا۟ أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ ٨٢ لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَءَابَآؤُنَا هَـٰذَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ ٨٣
{81-83} Yaani, bali makafiri hawa waliifuata njia ya watu wa mwanzo waliokanusha kufufuliwa, na wakaitenga kwa mbali kabisa, na wakasema: “Je, tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa?" Yaani, hili haliwezekani na haliingii akilini kwa mujibu wa madai yao. "Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani." Yaani, hatujaacha kuahidiwa kwamba ufufuo utakuwapo sisi na baba zetu, wala hatuuoni, wala haujafika bado. "Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani." Yaani, hadithi zao na tani zao ambazo huzungumza kuzihusu na hukengeuka, vinginevyo; basi hazina ukweli, na walikanusha akawefedhehesha Mwenyezi Mungu; kwani hakika Mwenyezi Mungu aliwaonesha kutokana na ishara zake kubwa kuliko ufufuo. Na mfano wake: "Bila shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu," "Na akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika... hadi mwisho wa aya. "Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapoyateremsha maji juu yake husisimka na kututumka... hadi mwisho wa Aya hizi.