المؤمنون
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَمَنِ ٱبْتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْعَادُونَ ٧
{7} "Lakini anayetaka kinyume cha haya" miongoni mwa asiyekuwa mke na suria, "basi hao ndio wavukao mipaka," ambao walivuka yale aliyohalalisha Mwenyezi Mungu hadi kwa yale aliyoharamisha, wale ambao wanayafanyia ujasiri maharamisho ya Mwenyezi Mungu. Na kwa ujumla, aya hii inaonyesha uharamu wa [nikah ya] Al-Mut'a. Kwa sababu mwanamke huyo siyo mke kihalisia anayekusudiwa kukaa wala kummiliki, na pia inaharamisha nikaha ya kumhalishia mke kuolewa na mke wake aliyekuwa amempa talaka zote tatu. Na inaashiria kauli yake, "wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia" kwamba, ili kijakazi awe halali, ni sharti awe amemilikiwa kikamilifu na mtu mmoja. Na ikiwa atakuwa amemmiliki baadhi yake tu, basi hawi halali kwake. Kwa maana, mwanamke kama huyo si katika wale uliomiliki mkono wake wa kulia, bali yeye ni miliki yake na ya wengineo. Kwa hivyo, kama vile hairuhusiwi kwa wanaume wawili kushiriki katika mwanamke huru, basi hairuhusiwi kwa mabwana wawili kushiriki katika kijakazi mmoja.